Video queen Bongo, Agnes Gerald maarufu kama ‘Masogange’ amejisalimisha katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mahakama hiyo ilitoa hati ya kukamatwa kwa Masogange baada ya kushindwa kuhudhuria mahakamani hapo mara mbili kwa ajili ya kusikiliza kesi yake inayomkabili ya matumizi ya madawa ya kulevya.

Kukamatwa kwa Masogange kulikuja baada ya upande wa mashtaka kuomba mahakama kutoa hati ya kumkamata kutokana mshtakiwa huyo na wadhamini wake kushindwa kufika mahakamani licha kuwepo kwa onyo.

Kutokana na ombi hilo Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbardi Mashauri alikubali ombi hilo na kutoa hati ya kukamatwa kwa Masogange.

Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.

Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14,2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *