Bondia Thomas Mashali anatarajiwa kuzikwa kesho siku ya jumatano katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Bondia huyo aliuwawa kwa kupigwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana maeneo ya Kimara jijini Dar es Salaam.

Baba mzazi wa Mashali amesema wameamua kufanya mazishi hayo Jumatano kwa kuwa wanapisha uchunguzi wa polisi.

Marehemu Mashali kabla ya kifo chake alikuwa  acheze na bondia Chimwemwe kutoka nchini Malawi pigano ambalo lilipangwa kufanyika mkoani  morogoro.

Mashali amezaliwa septemba 09 mwaka 1989 ameacha rekodi ya kushinda mapambano 19 kati ya hayo 9 akishinda kwa KO amepoteza mapambano 5 kati ya hayo amepigwa kwa KO mapambano 4 huku akitoka sare pigano moja tu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *