Mechi ya kirafiki kati ya Ivory Coast na Senegal imesimamishwabaada ya mashabiki kuingia uwanjani mjini Paris nchini Ufaransa.

Mashabiki wachache waliingia uwanjani huku mmoja akionekana akimrukia mchezaji wa Senegal Lamine Gassama.

Wachezaji walitoka uwanajania na refa Tony Chapron akaamua kusimamisha mechi hiyo kutokana na uvamizi huo.

coast

Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane alikuwa ameipa Senegal bao la kwanza mnamo kipindi cha pili, lakini Bi Gohi Cyriac akasawazisha dakika tatu baaadaye.

Hii ni mara ya pili ndani ya miaka mitano mechi kati ya chi hizo imesimamishwa kutokana na vurugu za mashabiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *