Imekuwa ni kawaida ya mastaa wa fani mbalimbali za burudani hapa nchini kujiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi miongoni mwao (wenyewe kwa wenyewe); sio tatizo kabisa as long as wao pia ni binadamu kama walivyo binadamu wengine.

Ingawa fani ya sanaa ya muziki na filamu ndizo zinazoongoza kwa kuwa na list ndefu ya mastaa wake ku-date lakini pia ndizo fani zinazoongoza kwa kuwa na mastaa ambao ‘mwanzo huwa huwa na mbwembwe nyingi na mwisho wao huwa na chuki zaidi’.

Lakini katika hali ya kuonyesha upevu wa fikra na hisia miongoni mwa wasanii hao wameendelea kuishi kwa wema na watu ambao kwa sasa hawana tena uhusiano nao na hata inapofikia hatua ya kuwaona waliopkuwa wapendwa wao wakiendelea na maisha mengine, wao pia hufurahi.

Hivi karibuni zilianza kuzuka tetesi kuwa Lil Samer a.k.a Mr. Blue a.k.a Byser ameingia kwenye biff na msanii anayekimbiza na ngoma yake SIWEZI, Barakah da Prince huku sababu inayotajwa kuwaingiza wawili hao kwenye biff kuwa ni mrembo NAJ.

Kwanini NAJ?

NAJ aliwahi kuwa mwandani wa Mr. Blue kwenye miaka ya nyuma lakini wawili hao wakaachana kutokana na sababu wanazozifahamu vizuri zaidi wao wenyewe lakini kwwa sasa Mr. Blue ni mume wa mtu na ni baba wa watoto wawili kutoka katika ndoa yake.

Upande wa pili, Barakah da Prince kwa sasa amezama mapenzini na mrembo NAJ na amefikia hatua ya kumvalisha ‘Promise ring’, kuwa ni yeye tu atakayemuoa, wakiendelea kuisubiri siku yenyewe.

Na hivi karibuni, Baraka da Prince akiwa na Ben Pol wameandaa ngoma ambayo ndani yake wamemshirikisha Mr. Blue na mzigo umeenda poa kabisa lakini kilichokuja kuzua uvumi huo ni kukosekana kwa picha ya Mr. Blue kwenye kava la promosheni la ngoma hiyo.

Kwa ustadi mkubwa na umahiri wa kuwamudu waandishi wa habari, Mr. Blue akakiri kushirikishwa kwenye ngoma hiyo na kukiri kukosekana kwenye kava hiyo na kudai sababu iliyopelekea kukosekana ni uharaka wa ufanywaji wa kava hiyo (siku 1) na kwa bahati mbaya yeye alikuwa safarini.

Kwanini uvumi utokee? Mashabiki tunapenda kuzua mambo na kuyapa taswira tunayoitaka sisi……Mr. Blue amekumbusha kuwa yeye ni mume wa mtu na baba wa familia yake ‘PERIOD’.

Kumbe kuna uhasama huwakuta wasanii kwa kuchonganishwa na watu ikiwemo mashabiki?

Congratulations Blue…You gotta family, you must respect it so should everyone else!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *