Mashabiki wa nyota wa filamu za Kichina Bruce Lee wamekosoa filamu mpya ya nyota huyo inayoelezea maisha yake.

Filamu hiyo ‘Birth of the Dragon’ inaonyesha maisha ya nyota huyo alipokuwa mdogo nchini Marekani pamoja na pigano lake lililozua utata dhidi ya Wong Jack Man mwaka 1964.

Filamu hiyo iliyoongozwa na George Nolfi ,ilionyeshwa kwa mara ya kwanza katika sherehe ya filamu ya Toronto.

Lakini mashabiki wengi wamepinga vile inavyomuonyesha Bruce Lee,wakisema kuwa nyota huyo alishushwa sana hadhi yake katika filamu inayozungmzia maisha yake yeye mwenyewe.

Mashabiki hao wamesema kuwa badala ya kusherehekea vile Bruce Lee alivyokuwa mnyama wamemfanya aonekane mtu muoga na mwenye wivu huku wakisema hii ni sawa na kushusha hadhi ya muigizaji huyo badala ya kuonyesha maisha yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *