Muigizaji wa vichekesho aliyejipatia umaarufu mkubwa kupitia Kundi la Vituko Shoo, Chrispine Lyogello ‘Masele Chapombe’ leo amefunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi, Specioza Malick.

Ndoa hiyo imefungwa katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Consolata lililopo Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam.

Desemba 23, 2016 Masele na Specioza walifanay send-off Moshi, Kilimanjaro, nyumbani kwa mwanamke.

Mchekeshaji huyo anakuwa msanii wa kwanza kufunga ndoa ndani ya mwaka 2017 kutokana na kufanya hivyo mapema kabla ya mwezi wa kwanza kumalizika.

Picha kwa hisani ya Global Publishers

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *