Muigizaji wa vichekesho nchini, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’ amewatembelea watoto waliopata ajali ya basi la shule ya Lucky Vicent waliopo Marekani kwa matibabu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Masanja Mkandamizaji ameposti picha akiwa na watoto hao na kuandika ujumbe ufuatao.

“Mungu amenipa neema ya kwenda kuwaona wadogo zetu waliopata ajali, Sadia na Wilson na kuwepo Marekani kwa matibabu….. Imekuwa siku njema kwetu sote tumefurahi pamoja nao kula nao na kumtafakari Mungu kwa pamoja.

Pia amendelea kwa kuandika “Lakini pia nimezungumza na wenyeji wao waliofanikisha safari ya wao kuja Marekani!! Hakika Mungu ni mwema wameendelea kuimarika na wanaendelea vizuri!!

Ameongeza kuwa “Shukrani kwa madaktari na kila aliyetenga muda wake kuwaombea,
wazazi wao wanawasalimu na wanawashukuru kwa ushirikiano na maombi yenu.”

 Watoto hao ni miongoni mwa wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent walionusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea mkoani Arusha mwezi Mei mwaka huu, ambapo inakadiriwa idadi ya waliopoteza maisha ni 33 ikijumuisha wanafunzi na walimu waliokuwa katika gari hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *