Serikali imepiga marufuku taasisi yoyote ya serikali kutoa taarifa inayohusu sakata la Faru John kwakuwa suala hilo lipo chini ya ofisi ya waziri mkuu na imeshaundiwa timu ya wataalam kulifuatilia hadi serikali itakapotoa taarifa.

Akiwa katika ziara ya siku mbili ya kikazi mji mdogo wa Loliondo wilayani Ngorongoro,Naibu waziri wa maliasili na utalii Ramo Makane amesema kumekuwa na mijadala inayoendelea kuhusu faru John na mengine imekuwa ikipotosha ukweli hivyo hakuna mtendaji au taasisi ya serikali itakayoruhusiwa kutoa taarifa hiyo na kusema kuwa suala hilo liko chini ya waziri mkuu.

“Lakini utaratibu wa kawaida wa kufanya kazi za serikali anayeagiza ripoti ndiyo mwenye ripoti, ripoti hii ya uchunguzi ni ya waziri mkuu, atakayeweza kuitoa ripoti hii nje ni waziri mkuu, hakuna mamlaka nyingine yeyote ya serikali chini ya waziri mkuu yenye uhalali wa kutoa tamko au kutoa ufafanuzi wa jambo hili,” alisema Makane.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *