Mbunifu wa mavazi mashuhuri nchini, Martin Kadinda amesema kuwa muigizaji nyota wa Bongo Movie, Wema Sepetu amebadilika sana baada ya kuacha tabia zake za hapoa awali.

Kadinda aliyekuwa meneja wa Wema amempongeza mwanadada huyo kwa kubadilisha mfumo wa maisha yake kinyume na matarajia yale.

Pia amesema kuwa kitendo cha Wema kufuta picha zake kwenye mitandao ya kijamii na kubadili tabia za kuweka wazi maisha yake ni hatua ya kupongezwa.

Kadinda amesema uamuzi alioufanya Wema ni hatua nzuri na ya kupongezwa kutokana na na familia yake haikuwa ikipendezwa na tabia yake kwa kuwa ilikuwa ikichafua jina lake.

Martin aliongeza kwamba Wema ambaye amebadili meneja kwa sasa amekuwa tofauti na alivyozoeleka maana amekuwa muelewa na msikivu kwa anachoelekezwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *