Mbunifu maarufu wa mavazi nchini, Martin Kadinda amesema kuwa hana ugomvi wowote na muigizaji wa Bongo movie, Wema Sepetu kama inavyodai na watu.

Kauli ya Kadinda imekuja kufuatia kwa taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii kuhusu kutoelewana wawli hao ambao ni marafiki wa muda mrefu na wamekuwa wakifanya kazi kwa pamoja.

Kadinda amesema kuwa watu wamezoea kukaa na kutengeneza mambo ambayo hayapo, yeye ni meneja wa Wema na ataendelea kufanya naye kazi kama kawaida bila tatizo lolote kwasababu wana mikataba katika kazi zao.

Mbunifu huyo amesema kuwa watu wamezoea kuzusha kila kukicha, kwa upande wake hajawahi kugombana na Wema ila watu wanataka kuwagombanisha hasa katika mitandao ya kijamii.

Kadinda aliongeza kwa kusema kuwa kwa sasa yuko bize na kazi zake za kubuni mavazi kama vile ya harusi ambayo yanamfanya azidi kuwa maarufu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *