Kocha wa zamani wa miamba ya soka ya Uingereza, Tottenham Hotspurs, Martin Jol ambaye alikuwa akiifundisha miamba ya soka ya Afrika, Al Ahly ameacha kazi ghafla na kukimbia nchini Misri kufuatia vitisho vya mashabiki.

Kocha huyo raia wa Uholanzi, ameacha kazi hiyo baada ya kuitumikia kwa miezi sita tu huku vitisho vya mashabiki wa timu hiyo juu ya usalama wake vikiongezeka.

Mashabiki wenye hasira wa klabu hiyo walimuonyesha hasira kocha huyo baada ya timu yao kutoka suluhu ya 2-2- na timu ya Zesco United ya Zambia na kutolewa kwenye mashindano ya Klabu Bingwa barani Afrika.

Jol alizozana na mashabiki Ijumaa iliyopita kufuatia suluhu hiyo na baada ya hapo aliendelea kupokea vitisho kupitia mitandao ya kijamii hali iliyopelekea kufanya uamuzi wa kuondoka nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *