Staa ghali zaidi kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 20, Anthony Martial, amekasirishwa na kitendo cha klabu yake ya Manchester United kutowasiliana nae kuhusu uamuzi wa kumpa jezi namba 9 staa mpya wa timu hiyo, Zlatan Ibrahimovoch.

Martial ambaye yuko likizo nyumbani kwao Ufaransa, alionyesha kwa vitendo kutokufurahishwa huko na kitendo hicho na kuamua kubadilisha picha aliyokuwa ameiweka kwenye mtandao wa Facebook iliyomuonyesha akiwa na jezi namba 9 ya klabu hiyo.

Manchester United wameamua kumpa Martial jezi namba 11 ambayo pia huivaa kwenye timu yake ya taifa ya Ufaransa huku jezi hiyo ikiwa pia imewahi kuvaliwa na magwiji wa United akiwemo Ryan Giggs.

Manchester United walizindua jezi mpya watakazozitumia kwenye msimu wa 2016/2017 juzi na staa mpya wa timu hiyo Zlatan Ibrahimovich aliionyesha jezi yake namba 9 kupitia mtandao wa Instagram.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *