Nyimbo mpya ya Diamond Platnumz aliyomshirikisha Ne-Yo imefikisha views Milioni 1 ndani ya siku tano.

Kutokana na rekodi hiyo Diamond Platnumz amekuwa msanii wa pili Tanzania kwenye mtandao wa VEVO kuwa na video iliyotazamwa zaidi ya mara 100 nyuma ya Vanessa Mdee ambae nyimbo zake mbili zimefikisha views zaidi ya Milioni 1.1.

Nyimbo hiyo ipo kwenye akaunti  mpya ya VEVO  na kuwa nyimbo ya kwanza kuwekwa kwenye mtandao huo.

VEVO ni mtandao wa internet unaoshughulika na video za muziki na wanamuziki unaomilikiwa na kampuni kubwa za muziki duniani SONY Music Group, Universal Music Group, Warner Music Group na Google.

Mtandao huo ni wa kwanza duniani unahusika na kuhifadhi na kurusha kazi za muziki za wanamuziki maarafu duniani, kama Jay Z, D’banji, Nick Minaj na Mafikizolo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *