Mmiliki wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg na mkewe Priscilla Chan ndio watu pekee ambao huwezi kuwablock katika mtandao wa Facebook.

Mwanzoni kabla ya Mark Zuckerberg kumuoa Priscilla ni yeye pekee ndiye ambaye hakukuwa na uwezekano wa Kumbloku.

Mark huandika taarifa nyingi kuhusu maboresho ya Facebook na taarifa mbalimbali kuhusu maisha yake binafsi au mambo mengine ya kijamii.

Kublock mtu ni njia mojawapo ya kutotaka mtu aone posti zako wala zake. Njia hii unaweza kufanya asiwe rafiki yako (Unfriend) au kukufuata (Unfollow)

Muanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg abadili mtazamo wake juu ya dini Mark Zuckerberg na Priscilla Chan  walikutana mwaka 2003 wote wawili wakiwa wanafunzi chuo kikuu cha Havard, na mwaka 2012 walioana baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa kipindi kirefu.

Kwa mujibu wa ripoti ndani ya The Independent, machapisho yote (ndani ya facebook) huonekana katika mifumo ya malekezo ya kitarakimu ya Facebook inayofahamika kama ‘algorithm’ na mwishowe kuzipeleka kwa wachangiaji mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *