Refa maarufu nchini Uingereza, Mark Clattenburg anatarajia kuondoka kwenye ligi ya nchi hiyo na kuelekea nchini Saudi Arabia.

Bodi ya waamuzi wa ligi kuu nchini Uingereza imesema kuwa mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 41 anaelekea Saudi Arabia kuwa mkuu wa kitengo cha waamuzi wa nchi hiyo.

Majukumu yake katika Shirikisho la soka nchini Saudi Arabia ni kuhakikisha timu za nchi hiyo zinafanya vizuri na kufanya ligi ya Saudi Arabia inakuwa ya kitaalamu zaidi.

Clattenburg mechi yake ya mwisho kuchezaesha katika ligi kuu ya Uingereza ilikuwa kati ya Arsenal na Hull City ambapo Arsenal ilishinda 2-0.

Ikumbukwe kuwa Clattenburg amechezesha Fainali kubwa tatu mwaka jana ya EURO nchini Ufaransa, fainali ya FA cup kati ya pamoja na Fainali ya Klabu bingwa Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *