Muigizaji nyota wa Hollywood, Marion Cotillard amevunja ukimya wake kuhusu talaka ya Brad Pitt na Angelina Jolie akikana kwamba ahusiki kuvunjika kwa ndoa ya wawili hao.

Muigizaji huyo maarufu nchini Ufaransa amesema hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Angelina Jolie na Brad Pitt
Angelina Jolie na Brad Pitt

Ameandika kama ifuatavyo ”Miaka mingi iliopita ,nilikutana na mpenzi wa maisha yangu.Yeye ndio penzi langu ,rafiki yangu na mtu ninayemuhitaji pekee’.

Cotillard pia alibaini kwamba yeye na mumewe Guillaume Canet walitarajia mtoto wao wa pili.

Maisha ya faragha ya msanii huyo mwenye umri wa miaka 40 yaliwekwa katika vyombo vya habari kufuatia habari kwamba Jolie alikuwa amewasilisha ombi la talaka kufuatia tofauti zisizotatulika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *