Kiungo wa Dortmund, Mario Gotze hatokuwepo kwenye mechi ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Benfica leo kutokana na kuumia goti.

Gotze ameumia kwenye mechi ya ligi kuu nchini Ujerumani dhidi ya Darmstadt amba walifungwa 2-1 kwenye mechi hiyo.

Nahodha wa Dortmund Marcel Schmelzer na Lukasz Piszczek ambao walikosekana kwenye mechi dhidi ya Darmstadt kutoka na majeraha lakini waatakuwepo kwenye mechi ya leo baada ya kupona majeraha.

Dortmund itarusha karata yake ya kwanza kwenye mechi ya klabu bingwa dhidi Benfica ikiwa ni hatua ya 16 bora ya michuano itakayoanza leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *