Mwanamuziki wa Hip-Hop nchini Marekani, Young Thug ametangaza kubadili jina lake hilo na sasa atajulikana kama Jeffery kwa mashabiki wake.

 Kiongozi Mkuu wa Lebo ya 300 Entertainment inayommiliki mwanamuziki huyo, Lyor Cohen amesema staa huyo sasa ataitwa kwa jina jipya la No, My Name Is Jeffery.

Cohen amesema kuwa uamuzi huo wa Thug umekuja ikiwa ni moja ya  mapinduzi katika kazi zake ambayo yanakuja na mixtape yake mpya iliyoko kwenye hatua za mwisho za maandalizi na ataichia hivi karibuni ambayo ameipa jina la  Jeffery.

Young Thugger kwenye mixtape yake hiyo mpya amewashirikisha mastaa kama vile Elton John, Birdman, Swizz Beatz, na bondia Floyd Mayweather Jr.

young-thug-square

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *