Marekani imetoa onyo dhidi ya mataifa ambayo yameonyesha kuiunga mkono Korea ya Kaskazini kwa kitendo chake cha kufanya majaribio ya silaha za nyuklia ambazo zimekuwa ni tishio kwa usalama wa dunia.

 

Kauli hiyo imetolewa na Balozi wa Marekani, Nikki Harley katika kikao cha dharula cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kuyapa tahadhari mataifa hayo yanayomuunga mkono Kora Kaskazini.

 

Balozi huyo amesema kuwa kitendo cha kuiunga mkono Korea Kaskazini si cha kiungwana, na kuongeza kuwa yatashghulikiwa kama yataendelea kufanya hivyo.  

 

Amesema kuwa ”Iwapo wewe ni taifa linalounga mkono Korea Kaskazini tutakutaja.tutahakikisha kila mtu anajua wewe ni nani na tutakuwekea vikwazo hata na kukushughulikia ”,.

 

Katika kikao hicho cha dharula cha Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kilifanyika mara baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio jingine la kombora la masafa marefu na kusema kuwa, jaribio hilo lilifanikiwa kwa asilimia 100.

 

Serikali ya Marekani inaunga mkono hatua za mazungumzo na nchi hiyo ili kuweza kuondoa tofauti zilizojitokeza katika hatua zinazofanywa na Korea Kaskazini kwani inahatarisha Usalama wa dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *