Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kujiondoa katika mpango wa Ushirikiano wa kiuchumi wa nchi zinazounganishwa na bahari ya Pasifiki.

Trump ameyaonya makampuni ya nchi hiyo yanayopeleka kazi nje ya nchi kwa kusema kuwa atayapa adhabu makampuni yatakayofanya hivyo.

Makubaliano ya Mpango wa Ushirikianio wa Kibiashara wa nchi zinazounganishwa na Bahari ya Pacific TPP, yalijadiliwa na utawala wa Rais Barack Obama.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sean Spicer amesema hatua hiyo ni dalili ya kuanza kwa enzi mpya ya sera za biashara za Marekani.

Amesema amri hiyo ya Rais inaongoza katika enzi mpya ya sera za biashara ya Marekani, ambayo utawala wa Trump utapata fursa ya kufanya biashara na washirika wake duniani kote.

Uamuzi huo ni taarifa ya kwanza ya utawala mpya wa Marekani kutoa kuhusiana na misaada inayotoa kimataifa.

Utawala unaongozwa na chama cha Republican nchini Marekani mara zote umekuwa ukipiga marufuku msaada wa serikali kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa ambayo yanatoa huduma za utoaji mimba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *