Ubalozi wa Marekeni nchini umeleta walimu 51 watakaofundisha masomo ya Sayansi, Hesabu na Mazingira kwa kipindi cha miaka miwili.

Katika hafla ya kuwaapisha walimu hao jijini Dar es Salaam, Kaimu Balozi wa Marekani Virginia Blesa amesema walimu hao watakaofanya kazi katika mikoa 22 watasaidia kupunguza tatizo la walimu wa masomo ya Sayansi nchini.

Bleisa amesema kuwa wapo walimu wengi wanatamani kufundisha kwa kujitlea nchini katika nyanja mbalimbali kupitia mpango wa kusaidia elimu ulioandaliwa na marekani kwa nchi masikini duniani.

Kwa upande wao walimu hao wamesema kuwa wanategemea wanafunzi watanufaika na elimu watakayowapa na kuomba ushirikiano kwa walimu watakaowakuta katika shule walizopangiwa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *