Marekani imekanusha madai kutoka kwa  Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan kuwa nchi hiyo imeisaidia kundi la wapigaji la waasi wa Islamic State (IS).

Msemaji wa serikali Mark Toner amesema madai hayo hayakuwa na msingi kutokana na Marekani kutohusika na msaada wowote kwa kundi hilo.

Kiongozi wa Urusi amesema kuwa ana idhibati tosha iliyoonyesha Marekani imetoa msaada kwa makundi ya KiKurdi ya YPG na PYD. Wanajeshi wa Uturuki wamekuwa wakipigana kuiondoa IS kutoka Kaskazini mwa Syria.

Wanajeshi 37 wa uturuki wameuawa katika oparesheni iliyoanzishwa mnamo Agosti kuwaondoa wanamgambo wa IS na wapiganaji wa Kikurdi kutoka eneo maalum lililoko karibu na mji wa al-Bab, ulioko kilomita 20 kutoka mpaka wa Uturuki.

Marekani imekuwa ikishirikiana na makundi ya Ki Kurdi nchini Syria lakini Uturuki inasema pia wanahusishwa na Chama cha wafanyikazi wa Ki Kurdi, (PKK), kilichokuwa kikiendesha juhudu za mapinduzi ndani ya Uturuki kwa muda mrefu.

Aidha, muungano unaowakilisha makundi ya waasi na upinzani nchini Syria, umeyarai makundi hayo kushirikiana na juhudi zinazoendlea ili kufanikisha maafikiano ya kusitisha mapigano.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *