Wakuu 70 wa chama cha Republican wamesaini barua na kuituma kwa mkuu wa kamati ya kitaifa ya chama hicho wakimtaka aache kusaidia kampeni za mgombea urais kupitia chama hicho, Donald Trump.

Barua hiyo imeeleza kwamba badala yake chama kinapaswa kuelekeza juhudi zake katika kuwalinda wagombea katika uchaguzi wa seneti na baraza la wawakilishi pekee.

Baadhi ya wajumbe wa zamani wa baraza la Congress nchini Marekani ni miongoni mwa waliosaini barua hiyo ya kuacha kumsapoti Bw. Trump.

Akijibu kuhusu hatua ya barua hiyo , Bw Trump amesema kuwa hajali kwamba chama kinaweza kukata msaada kwake na anamatumaini ya chama chake kumuunga mkono mpaka utakapofika uchaguzi huo.

Vile vile Trump amesema kwamba anachoweza kufanya ni kusitisha udhamini wake kwa chama cha Republican.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *