Rais mteule wa Marekani Donald Trump amekutana na Rais Barack Obama kwa mara ya kwanza ikulu ya White House tangu ashinde uchaguzi mkuu nchini humo.

 Trump kwenye kampeni zake alimweleza Obama kama rais mbaya zaidi kuwahi kuongoza Marekani.

Rais Obama naye amesema Mwanarepublican huyo hana sifa na uwezo wa kuwa kiongozi wa Marekani.

Mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York, ambaye sasa ni rais mteule kwa muda mrefu alitilia shaka uhalali wa habari kwamba Obama alizaliwa Hawaii na alikejeliwa hadharani na Rais Obama.

Wawili hao walishauriana kwa zaidi ya saa moja ofisi ya rais katika ikulu ya White House siku ya jana na walipojitokeza kwa wanahabari, walijaribu kuficha uadui kati yao.

Waliongea maneno mazuri kuhusu umoja na umuhimu wa kupokezana madaraka kwa amani.

Lakini picha zilizopigwa zinaonesha jambo tofauti, ukiangalia sura na mikono…

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *