Nchi za Marekani na China ambazo kwa pamoja huzalisha gesi chafu ya kaboni duniani kwa 40% zimekubali change mkono makubaliano yaliyopo kwenye mkataba wa hali ya hewa uliosainiwa kwenye mji mkuu wa nchi ya Ufaransa, Paris ujulikanao kama ‘Mkataba wa Paris’.

Baada ya kuwasili napamoja na viongozi wengine wa mataifa ya G20 kwa mkutano katika jiji la Hangzhou, rais wa Marekani Barack Obama amesema historia itahukumu juhudi za leo kama za la muhimu na mafanikio.

Kupunguzwa kwa gesi aina ya CO2 ndilo lengo linalotegemewa katika mabadiliko ya hali ya hewa.

Hatua kubwa kuelekea utekelezwaji wa makubaliano haya ilifikiwa mwezi Disemba, ambapo mataifa hayo yalikubaliana kupunguza gesi chafu kwa kiwango cha kuwezesha kupanda kwa joto la dunia kufikia chini ya nyuzi joto 2.

Mapema Jumamosi wajumbe wa kamati ya bunge la taifa la kongresi la watu wa Uchina- China’s National People’s Congress waliidhinisha “pendekezo la kuchunguza upya na kuidhinisha mapatano ya Paris ” Jumamosi asubuhi katika kilele cha wiki nzima cha vikao vya bunge.

Mkataba wa Paris ni mapatano ya kwanza kuwahi kuzingatiwa zaidi miongoni mwa makubaliano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Utekelezwaji wake utakubalika rasmi kisheria baada yakuidhinishwa na nchi 55 zinazozalisha 55% ya hewa ya Kaboni duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *