Staa wa mpira wa kikapu nchini Marekani, LeBron James atakuwa mchezaji anayepokea mkwanja mrefu kwenye ligi ya NBA msimu ujao baada ya kukubaliana na timu yake ya Cleveland Cavaliers kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu  ambapo atalipwa $100m (TZS 218bn).

Wakala wa mchezaji huyo, Rich Paul amesema kwamba James anatarajia kusaini mkataba huo mpya kwa ajili ya msimu uajo wa ligi ya NBA ambapo utamuweka kwenye timu hiyo mpaka msimu wa mwaka 2019.

Mchezaji huyo aliiongoza Cavaliers ambayo ni timu ya nyumbani kwake kushinda ubingwa wa kwanza wa NBA msimu uliopita baada ya kujiunga tena  na timu hiyo mwaka 2014.

LEBRON

James amesema kwamba amefurahishwa na fursa hiyo huku akidai kutetea taji lake la mchezaji bora pamoja na ubingwa wa NBA waliopata msimu uliopita.

James ambaye ni mchezaji bora mara nne wa NBA ameshinda mataji mawili ya ligi hiyo akiwa na Miami Heat kabla ya kurejea Cavaliers mwaka 2014.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *