Rais wa Marekani, Barack Obama amesema kuwa Mareakni itachukua hatua dhidi ya Urusi kwa madai kuwa ilihusika na kushwawishi uchaguzi wa urais nchini Marekani

Urusi inalaumiwa na Marekani kwa kudukua parua pepe ya chama cha Democratic na za msaidizi wa Hillary Clinton madai ambayo Urusi inayakanusha vikali.

Kwa upande wake  rais mteule, Donald Trump ametaja madai hayo kuwa yasiyo ya ukweli na yaliyochochewa kwa misingi ya kisiasa.

Mashirika ya ujasusi yanasema kuwa yana ushahidi wa kutosha kuwa wadukuzi wa Urusi walio na uhusiano na serikali waliendesha udukuzi huo.

Jana msemaji wa Ikulu ya White House amesema kuwa Rais Vladimir Putin alihusika na udukuzi huo.

Haijulikani ni hatua gani Marekani inanuia kuchukua, huku Obama akitarajiwa kuondoka ofisini tarehe 20 mwezi Januari mwakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *