Wagombea urais nchini Marekani, Hillary Clinton na Donald Trump wamezidisha kampeni kwenye majimbo yanayoshindaniwa sana huku kura za maoni zikionesha wamekaribiana sana zikiwa zimesalia siku chache kabla ya uchaguzi mkuu.

Wawili hao kwa mara nyingine wameshambuliana kwenye mikutano ya kampeni kila mmoja akisema mwenzake hafai kuwa rais.

Bi Clinton ambaye uongozi wake kwenye kura za maoni kitaifa unaonekana kufutika siku za karibuni amesema mpinzani wake wa chama cha Republican hawezi kudhibiti hisia zake na ana mtazamo hasi dhidi ya wanawake.

Bw Trump naye amesema Bi Clinton ataandamwa na uchunguzi wa jinai hadi ikulu ya White House.

Mgombea huyo anaonekana kuimarika dhidi ya Bi Clinton katika majimbo yanayoshindaniwa, kwa mujibu wa kura za maoni.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *