Lebo maarufu ya muziki nchini Marekani, Cash Money inayoongozwa na msanii Birdman imesaini mkataba na kampuni ya music ya Apple kwa ajili ya kusimamia kazi zao zote za muziki.

Mkataba huo hautawahusisha baadhi ya wanamuziki wa kundi hilo kama Lil Wayne na Nicki Minaj kwa kuwa wao walishasaini mkataba muda mrefu na kampuni ya Tidal inayomilikiwa na msanii Jay Z.

Mkataba huo ni wa kwanza wa kampuni hiyo kusaini kusambaza kazi za lebo nzima tofauti na ilivyozoeleka hapo awali walipokuwa wakisambaza kazi za msanii mmoja mmoja pekee lakini sasa wameamua kusambaza kazi za lebo nzima.

Kampuni hiyo pia inamiliki baadhi ya wasanii kama Drake, Taylor Swift, DJ Khaled na Future.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *