Gwiji wa soka wa Argentina, Diego Maradona amemkubali mtoto wake Diego Junior ambaye alikuwa naye mwishoni mwa wiki iliyopita huko Buenos Aires.

Diego Junior alizaliwa nchini Italia mwaka 1986 kutoka katika mahusiano ya pembeni aliyokuwa nayo baba yake lakini hakuwahi kukubalika rasmi na baba yake hata baada ya kulazimishwa kulipa fedha za matunzo yake na jaji wa mahakama ya Italia mwaka 1992.

Maradona mwenye umri wa miaka 55 sasa amemkubali rasmi mtoto wake huyo na kudai mbele ya wanahabari kuwa huyo ni mtoto wake wa kiume.

Maradona pia aliendelea kudai kuwa anadhani Diego Junior anafanana sana na yeye licha ya kukataa kufanya vipimo vya DNA kwa miaka kadhaa kufuatia kutakiwa kufanya hivyo na mahakama.

Naye Diego Junior aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuwa amefurahi hatimaye kukubaliwa na baba yake kwani yeye na mama yake waliisubiria siku hiyo kwa kipindi cha miaka 30

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *