Mkongwe wa soka nchini Argentina Diego Maradona ameeleza kukasirishwa kwake na kitendo cha mshambuliaji wa timu ya Argentina, Gonzalo Higuain kujiunga na miamba ya Italia Juventus.

Kwenye taarifa yake aliyoitoa kupitia mtandao wa Facebook, Maradona amekiri kuumizwa na kitendo hicho kwasababu Higuain anaihama Napoli na kujiunga na wapinzani wao Juventus.

Maradona ambaye aliwahi kuwa mshambuliaji wa Napoli ana akafanikiwa kutwaa taji la SERIE A na klabu hiyo, amelaumu biashara ya soka namna inavyowafanya wachezaji kuwaumiza mashabiki wao.

Maradona aliandika hayo baada ya kuvuja kwa taarifa kuwa mshambuliaji huyo anayewaniwa na vilabu vya Arsenal na Chelsea kuripotiwa kufanya vipimo vya afya chini ya viongozi wa Juventus huku akitarajia kumalizana na klabu hiyo ndani ya siku chache zijazo.

‘Suala la Higuain linaniumiza sana kwasababu anakwenda kwa wapinzani kabisa, lakini siwezi kumlaumu mchezaji. Mchezaji ana jukumu juu yake binafsi isipokuwa walafi wa fedha ndio wanaosababisha yote haya na kunufaika zaidi’. Ameandika Maradona.

 

Gonzalo: Akishangila moja ya goli lake kwenye mechi ya ligi kuu nchini Italia.
Higuain: Akishangila moja ya goli lake kwenye mechi ya ligi kuu nchini Italia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *