Mastaa wa Bongo, mkali wa Bongo Fleva Harmonize na mkali wa Bongo Movie, Jacquiline Wolper ‘wamerudiana’.

Ni dhahiri kuwa mastaa hao wameanza tena kurudi kwenye ‘headlines’ baada ya uhusiano wao kuvunjika mapema mwaka huu licha ya kuanza uhusiano chini ya mwaka mmoja.

Pamoja na kurudiana huko, Harmonize na Wolper wameamua kuweka wazi mambo kadhaa yaliyowafanya warudi tena kwenye ‘Love Story’ yao.

Wolper amebainisha kuwa licha ya kuwa mbali na Harmonize na kutangaza hadharani kuwa hana shida nae tena lakini mambo matatu yamemfanya aendelee kumfikiria na kuridhia kurudiana na staa huyo. Mambo hayo ni:

1:      Upole

2:      Ukarimu

3:      Kuijua dini (Uislam)

Ingawa jambo la tatu limekuwa likipata upinzani kutoka kwa mashabiki.

Wakati huo huo Harmonize nae amekanusha ‘LOVE STORY’ kuwa njia mbadala ya KUUZIA kazi zake mpya.

Harmonize amedai kuwa nafasi waliyonayo kwenye jamii ndio inayosababisha watu wafikirie hivyo lakini kimsingi ‘mapenzi yao ni kama mapenzi ya watu wengine wasiokuwa mastaa ambao kupendana kwao hakuhusiani na kazi zao’.

Hata hivyo, hivi karibuni Harmonize aliachia ngoma mpya, NIAMBIE ambayo alidai aliitunga wakati akiwa na Wolper na kabla mwezi haujaisha tangu kutoka kwa ngoma hiyo na kauli hiyo, wawili hao ‘wamerudiana’ sio KIKI?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *