Maofisa 14 wa utumishi wa Halmashauri za Momba, Tunduma, Mbozi na Ileje katika Mkoa wa Songwe wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuzalisha watumishi hewa na kuisababishia serikali hasara ya mamilioni ya fedha.

Kutokana na makosa hayo walikamatwa na kuwekwa rumande kwa siku nne kabla ya kutolewa kwa dhamana.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Luteni mstaafu Chiku Galawa, amethibitisha watendaji hao kusimamishwa kazi na kwamba hatua hizo zimechukuliwa na mamlaka zao za nidhamu.

Galawa amesema baada ya uchunguzi kukamilika hatua mbalimbali zitachukuliwa dhidi yao, ikiwemo baadhi yao kufikishwa mahakamani kwa kuwa baadhi ya makosa yaliyoainishwa na mamlaka zilizochukua hatua yanaonekana ni ya jinai.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *