Naibu Waziri wa Elimu, Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa wizara hiyo haihusiki na ajira za walimu nchini isipokuwa inafanya uhakiki wa taarifa za walimu wenye sifa za kuajiriwa Serikalini.

Mhandisi Manyanya amesema kuwa kwasasa wizara hiyo inapitia taarifa (CV) za walimu waliohitimu ngazi ya Stashada na Shahada na baada ya hapo itazituma taarifa hizo katika Wizara ya Utumishi ambao ndiyo wanaohusika na kuajiri.

Kuhusu wahitimu wa ngazi ya cheti, Manyanya amesema uhitaji mkubwa uliopo kwa sasa ni kwa walimu wa sekondari hususani wa masomo ya Phisics, Hisabati, Chemistry na Biolojia, hivyo inawahitaji kwa haraka zaidi walimu hao huku akisema wahitimu wengine ambao siyo wa masomo hayo na ambao siyo kwa ajili ya kufundisha sekondari, wasubiri utaratibu wa wizara inayohusika na utumishi.

Mhandisi Manyanya ameendelea kusema kuwa wanahitajika walimu wengi kuliko idadi waliyoitoa mwanzo na kuwataka wote waliotuma taarifa zao wawe na subira kwa kuwa mchako wa uhakiki bado unaendelea na majina yatatangazwa muda mfupi ujao ambao hautazidi kipindi cha miezi mitatu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *