Mwanamasumbwi mashuhuri, Manny Pacquiao wa Ufilipino anatarajia kupanda uliongoni dhidi ya bondia, Jeff Horn kutoka Australi ifikapo Aprili 22 mwaka huu.

Pacquiao alitangaza kusataafu mchezo huo lakini ameamua kurudui tena ulingoni kupambana na bondia huyo kutoka Australia.

Mapromota wa pambano hilo bado hawajaamua nchi gani wanamasumbwi hao watakutana na kuonesha makali yao lakini pendezo zipo kwa nchi za Australia, Marekani au nchi za Falme za Kiarabu katika bara la Asia.

Pambano hilo litavuta hisia za mashabiki kutokana na bondia Pacquiao kurudi ulingoni baada ya kutangaza kustaafu mchezo huo mapema mwaka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *