Bondia kutoka Ufilipino, Manny Pacquiao anatarajia kulejea ulingoni siku ya tarehe 5 Novemba kukabiliana na bingwa wa dunia, Jessie Vargas kutoka nchini Marekani.

Pacquiao mwenye umri wa miaka 37, bingwa wa zamani wa dunia ametangaza kwamba atarejea licha yake kutangaza kwamba angestaafu baada ya kumshinda Timothy Bradley mwezi Aprili mwaka huu.

Jessie Vargas
Jessie Vargas

Promota wake Bob Arum amesema mwezi uliopita kwamba mwanamasumbwi huyo kutoka Ufilipino angepigana tena mwaka huu.

Pacquiao na kundi lake watakutana 10 Agosti mjini Manila kuamua iwapo pambano hilo dhidi ya Vargas mwenye umri wa miaka 27 kama litaandaliwa Los Angeles nchini Marekani au Dubai.

Bondia Jessie Vargas alitwaa ubingwa mwezi Machi mwaka huu baada ya kumshinda Sadam Ali kutaka Marekani.

4000

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *