Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, amesema mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Jerry Muro yupo huru na anaendelea na kazi zote za klabu kama kawaida kutokana na kutokuwa na taarifa yoyote rasmi juu ya kifungo hiko.

Manji amesema Kama ni taarifa wamesikia kwenye magazeti na redio, kweli taasisi kama Yanga, msemaji wake anasimamishwa kwa njia hiyo.

Mwenyekiti huyo pia amesisitiza kuwa kama ni kweli basi TFF inapaswa kutoa hukumu ya kumfungia Muro kama ambavyo wamekuwa wakisikia katika vyombo vya habari.

TFF kupitia kamati ya nidhamu ilitangaza kumfungia Muro mwaka mmoja ikiwa ni pamoja na kumpiga faini.

Lakini TFF imekuwa ikisita kutoa hukumu yake inayohusiana na Muro, jambo ambalo linaifanya Yanga kuona kuna upotofu wa mambo na kukiukwa kwa usahihi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *