Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji ameunda Kamati mpya ya mashindano baada ya kujizulu kwa Isaac Chanji.

Isaac Chanji alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na akaiwezesha klabu kutwaa mataji yote matatu msimu uliopita huku wakiifunga Simba mechi zote na kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho alijiuzulu Mei mwaka huu.

Manji ametaja Kamati mpya chini ya Mwenyekiti, Mhandisi Paul Malume ambaye pia anaingia kwenye Kamati ya Utendaji kama Mjumbe Mteule.

Wajumbe wa Kamati hiyo ni Abdallah Bin Kleb, Mustafa Ulungo, Mhandisi Mahende Mugaya, Jackson Mahagi, Samuel Lukumay na Hussein Nyika.

Wengine ni Athumani Kihamia wa Arusha, Felix Felician Minja wa Mwanza, Leonard Chinganga Bugomola wa Geita, Omar Chuma, Hussein Ndama, Hamad Ali Islam, Yusuphedi Mhandeni, Beda Tindwa, Moses Katabaro na Roger Lemlembe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *