Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemuachia huru Yusuf Manji kwenye Kesi ya kuhujumu uchumi.

Hapo July 5 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ililazimika kuhamia kwa muda katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, na kumsomea mashtaka saba ya uhujumu uchumi, mfanyabiashara Maarufu Yusufu Manji na wenzake watatu.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya Manji kushindwa kufika mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka kutokana na kulazwa katika taasisi hiyo.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, jopo la Mawakili Waandamizi wa Serikali wakiongozwa na Mutalemwa Kishenyi, Nassoro Katuga na Tulumanywa Majigo.

Washtakiwa hao wanadaiwa walijipatia bidhaa isivyo halali mnamo Juni 30,2017 katika maeneo ya Chang’ombe A Temeke Jijini Dar es Salaam walikutwa na askari polisi wakiwa na mabunda 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) zenye thamani ya Sh milioni 192.5 ambazo zilipatikana isivyo halali.

Katika shitaka jingine inadaiwa washtakiwa hao walikutwa na mhuri wa serikali wa JWTZ isivyo halali Juni mnamo 30,2017 ambao umeandikwa” Mkuu wa Kikosi 121 kikosi cha JWTZ” bila ya kuwa na uhalali na kwamba kitendo hicho kinahatarisha uchumi na Usalama wa nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *