Aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yussuf Manji anashikiliwa na jeshi la Polisi kanda maalu ya Dar es Salaam.

Manji pamoja na ofisa wake mmoja wanashikiliwa tangu Ijumaa ya Juni 30, mwaka huu ambapo inadaiwa katika moja ya ghala la kampuni yake lilihifadhi sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Mfanyabishara huyo Casto Ngogo (35), ambaye anatajwa kukamatwa na Manji, alipandishwa kizimbani Juni 21, mwaka huu  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka ya kukutwa na sare za jeshi hilo zikiwmao suruali 5,000.

Inadaiwa kuwa Juni 15, maeneo ya Bandari Kavu ya Galco, Chang’ombe, Temeke, Dar es Salaam, Ngogo alikutwa na suruali hizo 5,000 za JWTZ kwenye kontena namba PCIU 82851 (5) zikiwa na thamani ya Sh milioni 59 mali ya Serikali bila kibali.

Hatua ya kukamatwa kwa Manji inatajwa kuwa ni sehemu ya kusaidia maelezo katika kesi hiyo ambapo anahusishwa kwa maghala yake kuhifadhi sare hizo za jeshi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *