Mfanyabiashara Yusuf Manji leo ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwamba yeye bado ni Diwani wa Mbagala Kuu na hatambui kuvuliwa udiwani.

Manji alitangazwa kuvuliwa udiwani na Meya wa Temeke, Abdallah Chaulembo September 6/2017.

Manji ametoa malalamiko hayo, kwenye kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili na wenzake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Katika kesi hiyo ambayo wakili wa serikali mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amedai upelelezi haujakamilika, Manji amedai ameona habari kupitia gazeti la Mwananchi kwamba amevuliwa udiwani.

Amedai kama ni kweli amevuliwa Udiwani hatambui, kwani ana miezi 2 yupo gerezani na serikali inatambua kwamba yeye ni Diwani.

Pia Manji amedai kuwa kama hilo haliwezekani, basi wamuandike barua itakayoonyesha agenda ya vikao vyote na yeye atazijibu kwa njia ya barua.

Pia amedai kuwa hiyo kesi ni nzito na DPP hapaswi kuangalia upande wake wa kesi tu, kwani yeye amechaguliwa na wananchi na anawasaidia.

Awali kabla ya kuelezwa hayo, wakili wa utetezi Seni Malimi alidai kuwa wanatarajia kuwasilisha maombi ambayo ni ya siri katika tarehe ijayo.

Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mashauri akautaka upande wa mashtaka kuhakikisha wanalifanyia kazi suala hilo, ambapo kesi imeahirishwa hadi September 18/2017.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *