Mfanyabiashara maarufu na mmiliki wa Quality Plaza na Mwenyekiti wa Yanga, Yusufu Manji ametakiwa kuripoti katika ofisi za uhamiaji  mkoani Dar es Salaam kutokana na kuajiri raia wa kigeni wasiokuwa na vibali vya kuishi nchini.

Afisa uhamiaji wa mkoa wa Dar es Salaam, John Msumule ametoa taarifa hiyo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu suala hilo.

Msumule amesema Manji anatakiwa kufanya hivyo kwa kudaiwa kuwa ameajiri watu wanaoishi nchini na kufanya kazi kinyume cha sheria.

Afisa amesema kuwa “Siku ya Ijumaa tulifanya upekuzi kwenye Jengo la Quality Plaza (linalomilikiwa na Yusuf Manji, lililopo Barabara ya Airport), tukakamata paspoti  126 ambapo paspoti 25 ndizo zina makosa, wamiliki wake hawana vibali  na wanafanya kazi kinyume na utaratibu, watapelekwa mahakamani pamoja na mwajiri wao, Yusuf Manji ili akajibu mashtaka hayo.

Aliongeza kuwa “Ilikuwa tumkamate jana lakini tukasikia kwamba amelazwa hospitali… hivyo akitoka hospitalini awasili haraka ofisi hii ili tumuunganishe kwenye kesi ya kuwaajiri watu wasio na vuibali.

Manji ambaye ni miongoni mwa watu waliotajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam wanaojihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya kwasasa amelazwa hospitalini akikabiliwa na tatizo la Moyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *