Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amefika kituo kikuu cha Polisi (Central) jijini Dar es Salaam kusikiliza tuhuma zinazomkabili za kujihusisha na madawa ya kulevya.

Manji ni miongoni mwa watu 65 waliotajwa kwenye orodha na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wanahojihusisha na uuzaji pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya ambao walitakiwa kufika kituoni hapo siku ya Ijumaa.

Baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kumtaja Manji kwenye orodha hiyo mwenyekiti huyo wa Yanga aliitisha kikao na waandishi wa habari kuelezea masikitiko yake ya kutajwa kwenye orodha hiyo.

Kwenye kikao hicho na waandishi wa habari, Manji amesema kuwa tuhuma hizo zimemchafua yeye pamoja na klabu yake ya Yanga na kusema kuwa yeye atahudhuria kituoni hapo leo na siyo Ijumaa kama alivyosema Makonda.

Mbali na Manji wengine waliotajwa kwenye orodha hiyo ni mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mchungaji Josephat Gwajima,  Aliyekuwa mbunge wa Kinondoni Idd Azzan pamoja na wengine ambao siyo watu maarufu sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *