Wakati kesi ya kuuwa bila kukusudia ikiendelea kumkabili Lulu, Mange amejitokeza na kumpa makavu muigizaji huyo kutokana na vitu anavyofanya.

Mange amedai vinaweza kupelekea mahakama kudhani kuwa hajali au haoni uzito wa mashataka yanayomkabili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange alimfungukia Lulu kuhusu matumizi yake ya mitandao ya kijamii kwa sababu anarusha picha kama kawaida haonyeshi kuwa yupo kwenye matatizo:

Lulu, uko mahakamani kwa kesi kubwa sana ya kuua bila kukusudia, achana na mitandao ya kijamii tafadhali. Sawa utaenda mahakamani na dera na kilemba lakini siku hizi majaji, makarani, wasaidizi wao na hata familia zao wako pia mitandaoni. Jaji akiamua kukufatilia kwanza ataona kama haujali na haujisikii vibaya kwa mashtaka yanayokukabili. Ukiachana na ukweli kuhusu kesi jinsi ulivyo, kumbuka jinsi ulivyo na Tabia unayoionyesha kipindi cha kesi huwa ni ishu. Jaribu kuwa Lulu uliyekuwa na wasiwasi na kutia huruma kipindi kile Kanumba alivyokufa au kama huwezi kuigiza mtu mwenye huzuni achana na mitandao ya kijamii kwa muda”.

Mange hakuishia hapo alimuonhealea Mama Kanumba na ugomvi wao ambao ni kosa kubwa alilofanya;

Kama kuna kosa kubwa ulifanya basi ni kumpotezea mama Kanumba! Amino Leo hii kungekuwa na uzito Mkubwa sana wewe kuingia mahakamani na mama wa marehemu. Jaji anaanzaje kusema una hatia wakati mama wa marehemu anasema wewe huna hatia? Lakini hushauriki Lulu nilikushauri sana juu ya hili suala la mama kanumba. Muombe Mungu wasimpandishe Mama Kanumba kizimbani! Kumbuka nchi nzima tulikuchukia lakini yule mama alikukumbatia, alichokufanyia yule mama hakilipiki kwa pesa yoyote hata kama alikukosea ulipaswa kumsamehe Mara 70. Sijui kwanini lakini mimi niliumia sana ulivyompotezea yule mama baada ya kesi yako kuisha makali yaani niliona Kama ulimtumia!”.

Kesi ya Lulu inategemewa kuendelea kuaikilizwa leo mambo yalimwia ugumu Jana Lulu baada ya kukutwa na kesi ya kujibu na hivyo kupandishwa kizimbani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *