Muigizaji nyota wa Bongo movie, Shamsa Ford ametumia akaunti yake ya Instagram kuelezea kinachomsibu mumewe Chid Mapenz ambaye anashikiliwa na polisi kutokana na kujihusisha na madawa ya kulevya.

Shamsa Ford ameeleza kuwa kabla ya kuolewa alijua ipo siku atapitia mitihani kama hiyo kwa hiyo yupo pamoja na mumewe huyo ambaye aamekumbwa na matatizo hayo.

Kupitia akaunti yake Shamsa ameandika kama ifuatavyo “nilipoolewa nilijua ipo siku nitapitia hivi vitu huzuni,furaha, maudhi, kudharauliwa, kuchekwa na nk.ila pamoja na yote hayo haitabadilisha mapenzi yangu kwa mume wangu kipenzi. Nina amini kuwa wewe ni mume aliyenipa Mungu na wala Mungu hakutukutanisha kwa bahati mbaya.Dunia nzima ikuzomee na kuamini kile wanachoamini lakini jua una mke anayekupenda kwa dhati .Ninakujua, ninakuamini na kukupenda sana ndomaana niliolewa na wewe kwasababu nilijua utakuwa baba bora kwa mwanangu kama ambavyo ulivyo sasa..Nina amini Mungu anapotaka kukupeleka sehemu anayoitaka yeye lazima akupitishe kwenye mitihani. Hii ni mitihani ya Mwenyezi Mungu na nina imani inshaallah yatapita..Nakupenda sana mume Wangu kipenzi Rashidi..”

Mfanyabiashara wa nguo jijini Dar es Salaam, Chid Mapenzi ni miongoni mwa washukiwa wa madawa ya kulevya waliotajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wiki chache zilizopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *