Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpozi amewakejeli mashabiki wa Arsenal baada ya kukosa nafasi ya kushiriki kombe la klabu bingwa Ulaya msimu ujao.

Ommy Dimpoz ambaye ni mshabiki wa klabu ya Manchester United amesema maneno hayo baada klabu hiyo ya Mashetani Wekundu kutwaa kombe la Europa Ligi na kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa msimu ujao.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Ommy ameandika kuwa ‘Arsenal msimu ujao haitashiriki klabu bingwa kwa sababu hawajaulamba akimaanisha kupendeza’.

Arsenal ambaye imemaliza nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi nchini Uingereza ivyo kusababisha kukosa nafasi ya kushiriki klabu bingwa Ulaya msimu ujao.

Jana Manchester United iliilza Ajax jumla ya magoli 2-0 kwenye fainali ya Europa ligi iliyofanyika nchini Sweden.

Magoli ya Manchester United jana yalifungwa na kiungo wake Paul Pogba aliyefunga goli la kwanza katika dakika ya 28 na goli la pili likafungwa na Mkhitaryan katika dakika ya 48 ya kipindi cha pili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *