Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kwamba haamini kwamba anacheza kamari kwa kuangalia zaidi ubingwa wa ligi ya Europa League.

Meneja huyo, ambaye ameamua kuangazia ligi hiyo badala ya kumaliza katika nafasi nne za kwanza Ligi ya Premia, anasema uamuzi wake ni wa busara.

United wanaongoza 1-0 dhidi ya Celta Vigo nusufainali kutoka kwa mechi ya kwanza wanapoelekea kwa mechi ya marudiano leo Alhamisi jioni uwanjani Old Trafford.

Mourinho amesema kuwepo kwa mechi nyingi ambazo klabu yake inahitajika kucheza kumemlazimu kuamua ataangazia wapi.

Mabingwa wa Europa League huhakikishiwa nafasi katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, sawa na klabu zinazomaliza naafsi nne za kwanza Ligi ya Premia.

Manchester United walishuka hadi nafasi ya sita baada ya jana Arsenal kuwalaza Southampton 2-0 Jumatano.

Arsenal waliwalaza United Jumapili katika mechi ambayo Mourinho aliwapumzisha wachezaji wengi wake nyota kwa ajili ya mechi ya leo.

Mourinho anaamini kwamba kushinda Europa League ndio njia nzuri zaidi iliyosalia ya kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Amesema hatakuwa na majuto kamwe iwapo watashindwa kutwaa ubingwa.”Hebu tusubiri tuone kama tutaweza.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *