Baada ya klabu ya Yanga kutangazwa mabingwa wa Tanzania Bara kwa mara tatu mfululizo Afisa Habari wa Simba, Haji Manara afunguka juu ya ubingwa huo.

Manara kupitia akaunti yake ya Instagram ameamua kuwakumbusha Yanga juu ya alama zao tatu walizopokonywa na TFF.

Manara amesema kuwa Simba hawajakata tamaa kuhusu kudai Point zao 3 walizokuwa wamepewa na baadae kupokonywa kwenye ishu ya mchezaji aliyecheza akiwa na kadi tatu za njano, huku akisisitiza kuwa Yanga watalipeleka Kombe msimbazi kwa magoti.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Manara ameandika ”Last week nilipowapongeza Yanga kwa ushindi na kuwaambia mapambano yanaendelea,sijui kama tulielewana!! Bila shaka sasa mmenielewa,,soon tutapewa haki yetu,MWANA KULITAKA,MWANA KULIPEWA.

Pia ameongeza kwa kuandika kuwa “Hivi unadhani FIFA wana figisu guys? kadi tatu za njano ni kukosa game inayofuata tu no way out!! ukizingatia reppti za mwamuzi na kamisaa na bodi inayosimamia ligi, sasa mjiandae kisaikolojia kulileta kombe kwa magoti! @Yangasc @simbasctanzania”.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *