Mwanamuziki wa hip hop Bongo, Harmorapa amemchana Master J kwa kusema hamtambui wala hadhani kama kama anaweza kuwa miongoni mwa ‘Producer’ walioweza ku-hit kwa ngoma kali Bongo.
Harmorapa anayetamba na wimbo wake wa ‘Kiboko ya mabishoo’ amefunguka hayo baada ya kutokea maneno makali ya mtayarishaji huyo kuwa Harmorapa hana kipaji cha muziki na kwamba si msanii bali analazimisha.
Kauli hiyo ya Master J ilionekana kuwachukiza baadhi ya wadau wa tasnia hiyo mpaka kupelekea meneja wake ambaye ni P. Funk kuingilia kati jambo hilo.
Kwa upande mwingine Harmorapa ametaja wasanii anaowakubali zaidi Bongo, amesema kwa upande wa hip hop anamkubali zaidi Fid Q na upende wa kuimba anamkubali zaidi Alikiba.
Kwa upande wa wasanii wa nje, amesema anamkubali za Lil Wayne, huku akimwagia sifa Diamond Platnumz kwa kuitangaza vyema Tanzania kimataifa.
Akizungumzia mafanikio aliyonayo mpaka hivi sasa tangu ajulikane, amesema kubwa kuliko yote ni heshima anayopatiwa na watanzania hata wale ambao hawakuamini kama ni msanii kweli, pia fursa ya kuaminiwa na kushauriana na wasanii wakubwa Bongo kama Juma Nature, Prof Jay na Mwana FA.
Pia amesema mafanikio mengine ni fursa ya kufanya kolabo na msanii kutoka nchini Ubelgiji anayefahamika kwa jina la Critical, ambapo amesema Mbelgiji huyo alilazimika kumlipa pesa Harmorapa ili kufanya naye kolabo.