Baada ya tukio la kutekwa mwanamuziki wa hip hop nchini Roma Mkatoliki juzi usiku, wasanii wenzake wameonesha kuguswa na tukio hilo.

 Mmoja wa wanamuzuki walioonesha kuguswa na tukio hilo ni mwanamuziki mwenzake wa hip hop Fid Q  kupitia ukurasa wake wa Instagram ameonesha hisia kali kutokana na tukio hilo.

 Fid Q kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa mamlaka ya usalama inatakiwa kufuatilia suala ili kujua watu hao wameenda wapi.

Nimeipokea hii HABARI kwa mstuko mkubwa.. sio tu kwasababu TONGWE ni moja kati ya wadhamini wetu wa #OpenMicThursday pia ni moja kati ya studio ambazo zimekua msaada mkubwa sana ktk kunyanyua vipaji na C E O @j_murder_tongwe amekua mstari mbele sana ktk kufanikisha hilo.

Fid Q ameongeza kwa kuandika “kinachonistua na kuninyima raha zaidi ni hili la hawa ndugu zetu akina @roma2030 @moni_centrozone Producer Belo na mlinzi kuwa hawajulikani waliko hadi hivi sasa.. ninaiomba MAMLAKA HUSIKA ya USALAMA itusaidie ili waweze kupatikana mapema na kuifutilia mbali ile hofu iliyotanda mioyoni mwa ndugu, jamaa na marafiki… mwisho namuomba MUWEZA WA VYOTE azifanyie wepesi familia za ndugu zetu waliopotelea kusikojulikana in sha Allah.

Roma Mkatoliki na wenzake wamekamatwa na hawajulikani wapi walipo wakiwa studio za Tongwe Records zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *